Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu TIN
Swali: Nini maana ya TIN?
Jibu: TIN ni namba ya utambulisho kwa mlipakodi.
Swali: Inatumika kwenye vitu gani?
Jibu: TIN inatumika kwenye matumizi ya biashara na yasiyo ya biashara.
Swali: Matumizi yasiyo ya biashara ni yapi?
Jibu: Matumizi hayo ni pamoja na ajira, umiliki wa chombo cha moto, leseni za udereva na kadhalika.
Swali: Kwa hiyo TIN inayotokana na ajira inakuwa siyo ya biashara?
Jibu: Ndiyo.
Swali: Kwanini imeletwa jambo hili mnalihitaji hivi sasa?
Jibu: Kila anayelipa kodi anapaswa kuwa na TIN na muajiriwa analipa kodi kutokana na ajira yake.
Swali: Inamaana kodi itaongezeka?
Jibu: Hapana, makato ya kodi yatakuwa yale yale.
Swali: Ikiwa mimi ninayo TIN tayari kuna haja ya kupata TIN kwa ajili ya ajira?
Jibu: Hapana, TIN hiyo ya mwanzo ndio itatumika na TIN huwa ni moja kwa mtu mmoja.
Swali: Mimi nina leseni ya udereva TIN yangu nitaijuaje?
Jibu: Fika katika ofisi yoyote ya TRA utapata TIN yako.
Swali: Ikitokea sina kabisa TIN?
Jibu: Unaweza kuipata kwa kuingia www.tra.go.tz kisha usajili wa TIN, weka namba ya NIDA na namba ya simu kisha jaza taarifa zako utapata TIN.
Swali: Ikiwa sina namba ya NIDA nafanyaje?
Jibu: Fika ofisi ya TRA na kitambulisho cha kura au barua ya serikali ya mtaa, utachukuliwa alama za vidole na kupata TIN yako.
Swali: TIN inapatikana kwa bei gani?
Jibu: TIN ni bure kabisa hakuna malipo yoyote.
Swali: Sasa ninayo ya biashara inatumika?
Jibu: Itatumika kwa sababu inayohitajika ni TIN.